Wednesday, October 10, 2018

Jipatie simu ya mezani (FWT) kwa bei nafuu. Ingia hapa kujionea bidhaa na ofa kedekede.

Rudi Nyumbani, Kumenoga.

Monday, September 24, 2018

Fursa zinazotolewa na ttcl coorparation njombe

  1. Mawakala wa Vouchers
    • TTCL Njombe inatoa fursa ya mawakala wa vocha ambao watasaidia kusambaza vocha mitaani ili wateja wetu wa line za simu za mikononi kurahisishiwa kupatikana kwa huduma za vocha.
    • Faida za kuwa wakala wa vocha

      1. Wakala wa vocha atauziwa kwa punguzo(discount) ya asilimia 10%.
      2. Mfano, vocha za thamani ya shilingi Tshs. 5,000/= atauziwa kwa Tshs. 4,500/= na kupata faida ya Tshs. 500/=.
      3. Na vocha ya thamani ya Tshs. 10,000/= atauziwa kwa Tshs. 9,000/= faida ni Tshs. 1,000/=.
      4. Na vocha za thamani ya Tshs. 100,000/= atauziwa kwa gharama ya Tshs. 90,000/= faida ni Tshs. 10,000/=.
  2. Freelancers
    • Pia wanahitajika vijana ambao watakuwa wanasajilisha line za TTCL kwa wateja wetu kuwarudisha nyumbani. Hii ni fursa inatolewa kwa vijana wetu inasaidia kupunguza vijana wa mitaani ambao hawara kazi. Na kuwapatia ajira.
    • Manufaa ambavyo atapata Freelancer

      1. Akimsajilia line moja kwa mteja analipwa 500/=.
      2. Mteja akiweka vocha analipwa asilimia 30% ya vocha ya mteja.
      3. Pia atalipwa asilimia 30% ya matumizi ya mteja kwa mwezi.
    • Mtu akihitaji kuwa freelancer afike ofisini kwetu Njombe TTCL mkabala na Ofisi ya Posta akiwa na moja kati ya vitambulisho hivi:-
      1. Voter's ID (Kitambulisho cha kupigia kura)
      2. Driving licence (Leseni ya udereva)
      3. Nation ID (Kitambulisho cha Taifa)
      4. Passport (Pasipoti ya kusafiria)
      5. Kitambulisho cha Mkazi Zanzibar
  3. Mawakala wa T-PESA

    • Pia tunahitaji mawakala wa T-PESA maeneo mbalimbali ili watusaidie kufikisha huduma zetu za kifedha ambapo watu wanaweza kufanya miamala ifuatayo:-
      1. Kutuma pesa
      2. Kutoa pesa
      3. Kuweka pesa
      4. Kulipa bili mf. Tanesco, Ving'amuzi n.k.
      5. Lipa muuzaji
      6. Huduma ya vifurushi
    • Sifa za muombaji wa kuwa wakala wa T-PESA
      1. Awe na leseni ya biashara ambayo haijaisha muda wa kutumika
      2. Awe na Taxpayer Identification Number (TIN) i.e. Namba ya mlipakodi; ya TRA
      3. Awe na kitambulisho kati ya hivi:-
        • Voter's ID (Kitambulisho cha kupigia kura)
        • Driving licence (Leseni ya udereva)
        • Nation ID (Kitambulisho cha Taifa)
        • Passport (Pasipoti ya kusafiria)
        • Kitambulisho cha Mkazi Zanzibar
    • Namba ya wakala inatolewa bure bila malipo yoyote ukiwa na kianzio cha Tshs. 50,000/=.